Najua kama wewe ni mmoja kati ya wapenda soka, basi jina la mchambuzi wa soka mkongwe Dr Leaky litakuwa sio geni masikioni mwako, Dr Leaky ambaye tutaanza kumuona tena msimu huu kupitia TV 1 ambao wamepewa mamlaka ya kuonesha Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017 ametabiri Bingwa EPL kabla hata ya Ligi Kuanza.
Dr Leaky ametabiri bingwa Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017 itakuwa ni klabu ya Man City inayofundishwa na Pep Guardiola “Mwaka huu nafikiri Bingwa wa EPL atakuwa ni Pep Guardiola kwa mfano kama ni wale wat wa betting huwa wanaangalia vigezo vingi, lakini Guardiola nasema atakuwa Bingwa kutokana na kikosi alichonacho”
ALL GOALS: SIMBA VS COASTAL UNION FA CUP APRIL 11 2016, FULL TIME 1-2