Baada ya kuanza msimu bila kufungwa, kabla ya Newcastle United kuvunja rekodi yao wiki iliyopita kwa kuifunga 2-1, sasa leo Jose Mourinho aliingiza timu yake uwanjani kucheza dhidi ya Hull City.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Chelsea – Stamford Bridge umemalizika kwa ushindi mwingine kwa watoto wa tajiri Roman Abramovich.
Eden Hazard na Diego Costa waliifungia Chelsea magoli hayo na kuihakikishia timu hiyo nafasi ya kuendelea kuongoza ligi kuu ya England.
Katika mchezo mwingine Man City imefanikiwa kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Leicester City.
Frank Lampard alifunga goli la ushindi.