Klabu ya Chelsea ambayo ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Uingereza, December 5 wameshuka dimbani kucheza mchezo wao wa 15 wa Ligi Kuu Uingereza na kuendelea na harakati za kujikwamua kutoka nafasi za chini katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza.
December 5 Chelsea ilicheza dhidi ya Bournemouth katika uwanja wake wa nyumbani na kukubali kipigo cha goli 1-0 mbele ya Bournemouth, kwa goli pekee lililofungwa na Glenn Murray dakika ya 82 ya mchezo. Kwa matokeo hayo Chelsea ambayo ipo nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi, inakuwa imepoteza jumla ya mechi 8.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu Uingereza December 5
- Arsenal 3-1 Sunderland
- Man Utd 0-0 West Ham
- Southampton 1-1 Aston Villa
- Swansea 0-3 Leicester
- Watford 2-0 Norwich
- West Brom 1-1 Tottenham
Video ya magoli ya Chelsea Vs Bournemouth
https://youtu.be/VwZ4BXx16oQ
Video ya magoli ya Arsenal Vs Sunderland
https://youtu.be/8t45X2BtP54
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.