Mtu wangu mpenda soka najua ungependa kufahamu matokeo ya muendelezo wa mechi nne za Ligi Kuu Uingereza zilizochezwa Jumapili ya November 29. Leo zilipigwa mechi nne tu za Ligi Kuu Uingereza miongoni mwa mechi zilizopigwa November 29 ni mechi kati ya Norwich City dhidi ya Arsenal katika dimba la Carrow Road.
Arsenal waliingia uwanjani wakiwa wanacheza mechi yao ya pili mfululizo ugenini, baada ya wiki iliyopita kukubali kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa West Brom, mchezo uliochezwa katika dimba la The Hawthorns lenye uwezo wa kuchukua zaidi ya mashabiki 26,000, kabla ya November 29 Arsenal kulazimishwa sare ya goli 1-1 na Norwich City na weekend iliyopita kupokea kipigo.
Licha ya kuwa Arsenal walikuwa mahiri uwanjani kwa kufanikiwa kumiliki mpira kwa asilimia 63 na Norwich City asilimia 37, walishindwa kulinda goli lao lililofungwa na Mesut Ozil dakika ya 30 kipindi cha kwanza na Norwich City walifanikiwa kusawazisha goli hilo dakika ya 43 kupitia kwa Lewis Grabban.
Matokeo ya mechi za Ligi Kuu Uingereza zilizochezwa November 29
-
Tottenham Hotspur 0 – 0 Chelsea
-
West Ham United 1 – 1 West Bromwich Albion
-
Liverpool 1 – 0 Swansea City
Video ya magoli ya mechi kati ya Norwich City Vs Arsenal
https://youtu.be/Hb8DHryt4L8
Video ya magoli ya Liverpool Vs Swansea City
https://youtu.be/A4xoyXCVtS8
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.