Weekend ya burudani ya soka kwa Ligi Kuu Uingereza ilimalizika usiku wa February 14, kwa jumla ya michezo mitatu kuchezwa kwa siku hiyo, klabu ya Manchester City na Tottenham Hotspurs ndio vilimaliza weekend ya burudani ya soka kwa kucheza mchezo wao katika dimba la Etihad, wakati ambao vilabu vya Arsenal, Leicester City, Liverpool na Aston Villa vilikuwa vimecheza michezo yao weekend hiyo.
Man City ambao walikuwa katika dimba lao la nyumbani, safari hii wamekutana na kichapo goli 2-1 kutoka kwa Tottenham Hotspurs, licha ya kuwa walikuwa kwao, Spurs ndio walikuwa wa kwanza kupachika goli dakika ya 54 kwa mkwaju wa penati kupitia kwa mshambuliaji wao wa kutumainiwa Harry Kane, kabla ya Man City kusawazisha dakika ya 74 kupitia kwa Kelechi Iheanacho, Spurs walifanikiwa kufunga goli la ushindi dakika 7 kabla ya mchezo kumalizika kupitia kwa Christian Eriksen.
Kwa matokeo hayo Sputs wametimiza jumla ya point 51 sawa na Arsenal, ila wao wamefanikiwa kuwa nafasi ya pili kwa tofauti ya magoli na Arsenal kuwa nafasi ya tatu wakiwa sawa wote wamecheza michezo 26, wakati Man City wapo nafasi ya 4 wakiwa sawa kimichezo na Spurs ila wao wana point 47.
Video za magoli ya mechi ya Manchester City 1 – 2 Tottenham Hotspur
https://youtu.be/KqQ6pqszQAQ
Video ya magoli ya mechi ya Aston Villa 0 – 6 Liverpool
https://youtu.be/U6A0RRrsLuI
Video ya magoli ya Arsenal 2 – 1 Leicester City
https://youtu.be/Pusa05W1n4E
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE