Klabu ya Swansea November 9 2014 imeendeleza ubabe mbele ya vilabu vikubwa vya ligi kuu ya Uingereza ambapo wakicheza kwenye uwanja wao wa Liberty, Swansea ambao waliwafunga 2-1 Man United kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi hiyo, wamewachapa Arsenal 2-1.
Gunners walianza kupata goli la kuongoza kupitia mchezaji wao nyota Alexis Sanchez katika dakika ya 63 lakini yuleyule mchezaji aliyewaliza Man United Gylfi Sigurdsson akaisawazishia Swansea kwenye dakika ya 74.
Akitokea benchi Mshambuliaji Bafetimbi Gomez alifunga goli la ushindi dakika mbili kabla ya mechi kuisha hivyo mpaka mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho jahazi la Arsene Wenger na vijana wake lilikuwa limezama.
MSIMAMO WA LIGI
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook