Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema Hamas sio shirika la kigaidi bali ni kundi la ukombozi linaloendesha vita kulinda ardhi yake.
Katika hotuba yake kwa wabunge wa chama chake bungeni, Bw Erdogan alisema Israel ilichukua fursa ya nia njema ya Uturuki na kwamba hatakwenda Israel kama ilivyopangwa awali.
Alitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja kati ya Israel na Hamas na kuzitaka mataifa yenye nguvu duniani kuishinikiza Israel kusitisha mashambulizi yake dhidi ya Gaza.
“Wao (Hamas) wanajaribu kuokoa watu wao na nchi yao,” Erdogan aliongeza, akitangaza kundi lililoteuliwa kama kundi la kigaidi na Marekani, Uingereza na Israel kama “kundi la ukombozi”.
“Sasa tumeghairi ziara zetu za majimbo nchini Israel. Hatuna tatizo na taifa la Israel, lakini kamwe hatutakubali kufanya ukatili,” Erdogan alisema.
“Israel haijitetei, lakini inatenda uhalifu dhidi ya ubinadamu. Dunia nzima lazima ichukue hatua kukomesha vitendo hivi vya kinyama.”