Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kwa mara nyingine tena ametoa wito kwa Israel kuwajibika kimataifa kuhusu mwenendo wake huko Gaza pamoja na kudai kuwa waziri mkuu huyo atahukumiwa kama mhalifu wa kivita.
Akizungumza katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), rais wa Uturuki pia alisema kuwa Gaza ni ardhi ya Palestina na daima itakuwa ya Wapalestina.
Amekuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Israel tangu vita hivyo kuzuka, huku akiutuhumu mara kwa mara utawala wa Benjamin Netanyahu kwa kuvunja sheria za kimataifa, pamoja na kukataa kuita Hamas kuwa shirika la kigaidi.
Jeshi la Israel limepanua mashambulizi yake ya angani na ardhini kwenye Ukanda wa Gaza, ambao umekuwa chini ya mashambulizi ya angani tangu mashambulizi ya kushtukiza ya kundi la Palestina Hamas tarehe 7 Oktoba.