July 28 201 7 Mahakama ya Rufaa ilitupilia rufani iliyofunguliwa na wapiga kura wa jimbo la Bunda mjini katika kesi ya uchaguzi wa kupinga matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa jimbo hilo, Ester Bulaya.
Wapiga kura hao ambao wanampigania aliyekuwa Waziri wa Chakula, Kilimo na Ushirika na mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Bunda Mjini, Stephen Wasira, wapo wanne ambao ni; Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malagila.
Uamuzi huo umetolewa na Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Elizabeth Mkwizu ambapo amesema, upande wa walalamikaji uliwasilisha hoja 10 za kupinga ushindi wa Bulaya, lakini hoja hizo hazikuwa na mashiko, hivyo zinatupiliwa mbali.
Miongoni mwa hoja zao ni “Stephen Wassira, hakualikwa katika mchakato wa kujumlisha kura suala hili linaweza kuathiri matokeo ya uchaguzi kwa kushindwa kumtambua mgombea wala chama chake,” Sasa baada ya ushindi huo AyoTV na millardayo.com imempata Ester Bulaya anazungumzia ishu ya gharama alizotumia kipindi cha kesi yake na kingine ni mambo mawili ambayo hatayasahau kwenye kesi hiyo……..
“Ukishamuona wakili mwenyewe ni Tundu Lissu, wewe ukishamuona wakili mwenyewe ni ghali lakini gharama sio tu kwa wakili, kuna gharama ya kusafiri pia kuna watu wananizunguka na wanakuwa wananiunga mkono kwa wakati wote nakuwa nao kwa hiyo ni mkwanja mrefu nimetumia, ni zaidi ya milioni 100 kwa kipindi chote cha kesi”-Ester Bulaya
VIDEO: Lissu alivyofunguka ishu ya kutaka kupimwa mkojo na mengine, Bonyeza play hapa chini kutazama