Mbunge wa Bunda Mjini Estar Bulaya, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa ndoa yake na mumewe Gustavu Babile haijavunjika na anaishi Mbweni, Dar es Salaam.
Bulaya ameyaleza hayo wakati akijibu maswali ya Wakili wa Serikali, Mwandamizi Simoni Wankyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
Wakili Wankyo alimuuliza Bulaya kwamba ni sahihi ndoa yake ilivunjika.
Katika majibu yake amedai kuwa walifunga ndoa mwaka 2003, pia ndoa ya Kanisani haivunjiki na kwamba Halima Mdee ni jirani yake huko Mbweni.
Akihojiwa na wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi, kuhusu hati yake ya kusafirià amedai, katika hati hiyo hakuna màhali popote palipogongwa mhuri pakionesha alisafiri nje ya nchi kati ya Februari 16 hadi 28 mwaka 2018.
Amedai alichoieleza mahakama ni kwamba, Februari 16 mwaka jana 2018 aliwahi kuondoka katika Mkutàno wa kufunga kampeni kwakuwa Mdee alikuwa anaumwa hivyo walienda kujiandaa na safari ya kwenda kwenye matibabu Afrika Kusini.
Mkutano huo wa kufunga Kampeni ulifanyika katika viwanja vya Buibui, Mwananyamala Dar es Salaam.
Amedai hajawahi kuieleza mahakama siku waliyosafiri na katika hati yake ya kusafiria imegongwa mhuri katika ukurasa wa 17.
Katika hatua nyingine alidai, hakuna sheria inayoruhusu chama cha siasa kuhamasisha wafuasi wake kudai haki kwa maandamano ama vurugu.
Baada ya kueleza hayo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 20 hadi 24 mwakani 2020 àmbapo shahidi wa 10 wa upande wa utetezi ,anataràjiwa kutoa ushahidi wake.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe, Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika na Àliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Vicent Mashinji.
Wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Dokta Vicent Mashinji ambaye ni ,Katibu Mkuu taifà wa chama hicho na Ester Matiko.
Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.
Pia wanadaiwa kuwa Februari 16, 2018 katika barabara ya Kawawa Kinondoni Mkwajuni washitakiwa hao wakiwa na wenzao ambao hawapo mahakamani walikiuka tamko la kuwataka kutawanyika la Afisa wa polisi SSP, Gerald Ngiichi kwa kugoma kutawanyika na kupelekea uvunjifu wa amani.
Inadaiwa kugoma huko kulipeĺekea hofu na hatimaye kusababisha kifo cha Akwilina Akwiline na majeruha kwa askari wawili ambao ni H.7856 PC Fikiri na E.6976 CPL Rahim Msangi.