Kinda wa Arsenal Ethan Nwaneri anatazamiwa kusaini mkataba wake wa kwanza wa kikazi na klabu hiyo wiki ijayo, gazeti la Daily Mail linaripoti.
Chelsea na Manchester City zote zimeonyesha nia ya kumnunua kiungo huyo, ambaye alikua mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kutokea katika Premier League alipotokea msimu uliopita akiwa na umri wa miaka 15 na siku 181.
Nwaneri alifikisha umri wa miaka 17 siku ya Alhamisi, na hivyo kumfanya astahili kusaini mkataba kamili na klabu hiyo atakaporejea kutoka Uingereza U17.
Arsenal hivi majuzi imewasainisha mabeki Ben White na Takehiro Tomiyasu kwa kandarasi mpya ya muda mrefu huku The Gunners wakielekea kuwashikilia wachezaji wao muhimu.