kumekuwepo na mapigano tangu Jumatano asubuhi kati ya wanamgambo na vikosi vya serikali katika mji mtakatifu wa Ethiopia wa Lalibela (kaskazini), ulioko katika eneo linalokumbwa na vita la Amhara na maarufu kwa makanisa yake yaliyochongwa mwamba, kulingana na wakaazi kadhaa.
Wanamgambo wa “kujilinda” wa Amhara Fano waliunga mkono jeshi la Ethiopia wakati wa mzozo wa miaka miwili kati yake na viongozi wa waasi wa mkoa jirani wa Tigray, ambao ulimalizika kwa makubaliano yaliyotiwa saini Novemba 2022 huko Pretoria.
Makubaliano haya, yanayoonekana kama mabadiliko ya muungano, yalizidisha mivutano huko Amhara, ambayo ilibadilika na kuwa mzozo wa wazi wakati serikali ya shirikisho ilipojaribu mwezi Aprili kupokonya silaha vikosi vya kikanda.
“Mapigano yalianza leo asubuhi mwendo wa saa 08:00 (05:00 GMT) na milio ya risasi bado inaendelea kusikika. Inaonekana Wafano wanadhibiti baadhi ya maeneo ya mji, naona vikundi vidogo kwenye barabara kuu”, shemasi katika mji huo aliiambia AFP kwa njia ya simu, akiomba kutotajwa jina kwa sababu za kiusalama.
Haijawezekana kuthibitisha madai haya kwa kujitegemea, kwa kuwa mamlaka ya shirikisho yanazuia ufikiaji wa Amhara.
Si serikali ya shirikisho wala jeshi la Ethiopia lililojibu mara moja jumbe kutoka kwa AFP.
Mkazi mwingine aliyewasiliana na AFP, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema pia kwamba mapigano yaliyoanza mwendo wa saa 8.00 asubuhi yanaendelea na kwamba Fano wanaonekana mjini humo. Alituhakikishia kwamba hakuna mapigano yoyote yaliyotokea Jumatano karibu na makanisa ya rock, eneo la Urithi wa Dunia wa UNESCO.