Mshambuliaji wa zamani wa Cameroon na Barcelona Samuel Eto’o amekiri kosa la ulaghai wa kodi ya pauni milioni 3.2 inayotokana na haki yake ya picha alipokuwa akiichezea Barcelona.
Mwanasoka huyo bora wa mwaka wa Afrika mara nne alihukumiwa kifungo cha miezi 22 jela alipofikishwa mahakamani nchini Uhispania siku ya Jumatatu. Ni lazima alipe pesa anazodaiwa, pamoja na faini ya £1.55m.
Waendesha mashtaka walimshutumu Eto’o kwa kushindwa kutangaza mapato kutokana na uhamishaji wa haki za picha kati ya 2006 na 2009.
Eto’o ni mmoja kati ya orodha ndefu ya wachezaji na mameneja wa kigeni kufunguliwa mashitaka ya ulaghai wa kodi nchini Uhispania katika miaka ya hivi karibuni, wakiwemo Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Jose Mourinho na Neymar.