Nchi za Umoja wa Ulaya Jumatatu zilikubali kuongeza kiwango cha juu zaidi cha misaada inayotumika kufadhili msaada wa kijeshi kwa Ukraine kwa euro bilioni 3.5 (dola bilioni 3.8) hadi bilioni 12,na tayari kimetenga takriban euro bilioni 4.6 kama msaada wa kijeshi kwa Ukraine.
Uamuzi huo utahakikisha tena kwamba kuna fedha za kuendelea kutoa msaada wa kijeshi kwa vikosi vya washirika wetu, mwanadiplomasia wa juu wa kundi hilo, Josep Borrell, ambaye alikuwa ameomba fedha ziongezwe, alisema katika taarifa.
‘Kituo hiki kimethibitisha thamani yake imebadilisha kabisa jinsi tunavyounga mkono washirika wetu juu ya ulinzi, hii inafanya EU na washirika wake, kuwa na nguvu’, aliongeza kusema hivyo.
Waziri wa mambo ya nje wa Hungary, Peter Szijjarto alisema siku ya Jumatatu kuwa haitaondoa kizuizi cha dola milioni 546 za mfuko uliopo, hadi Kyiv itakapoondoa benki ya Hungary iliyoorodheshwa OTP kutoka kwenye orodha ya makampuni Kyiv ikiita wafadhili wa kimataifa wa vita vya Russia nchini Ukraine.