Umoja wa Ulaya EU umetangaza safari ya ndege ya kibinadamu kuelekea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kusafirisha vifaa vilivyohitajika sana katika mji wa Goma kwa matumizi ya kibinadamu.
Umoja wa Ulaya unasafirisha tani 180 za chakula, dawa na vifaa vingine kwa kutumia ndege mbili kutoka Ulaya hadi mji mkuu wa Kenya Nairobi.
Kutoka Nairobi, jumla ya ndege nane zitasafirisha misaada hiyo hadi Goma, huku mbili kati ya hizo ndege, zikiwa tayari zimewasili mjini Goma siku ya Jumanne.
Aidha kwa mujibu wa EU Wafanyakazi wa kibinadamu wanaosambaza misaada na usaidizi kwa raia katika majimbo hayo wanahitaji ufadhili zaidi na vifaa vya matumizi.
Itakumbukuwa kuwa kati ya mzewi Machi na Mei mwaka huu EU ilituma ndege 7 nchini DRC ikiwa na tani 260 za msaada kwa ushirikiano na Ufaransa na mashirika ya kibinadamu.
Msaada wa hivi punde kutoka kwa EU kwenda nchini DRC inakadiriwa kuwa euro milioni 80.