Umoja wa Ulaya umethibitisha kusitisha kwa muda malipo kwa shirika la mpango wa chakula duniani WFP kwa ajili ya kutoa misaada ya kibinadamu nchini Somalia.
Msemaji wa tume ya Umoja wa Ulaya, Balazs Ujvari, amesema hatua hiyo imechukuliwa kama njia moja ya kulinda fedha za Umoja huo.
Uchunguzi uliofanywa na Umoja wa Mataifa ulibaini kuwepo kwa wizi wa misaada inayotolewa nchini Somalia kwa ajili na maofisa katika taifa hilo, maofisa wa usalama ambapo pia wafanyikazi wa misaada wanahusishwa na sakata hilo.
Mwaka jana Umoja ya Ulaya ulitumia zaidi ya Dolla milioni saba sawa na pauni milioni 5.6 kwa ajili ya kuendeleza shughuli za shirika la mpango wa chakula duniani WFP nchini Somalia.
Mwaka jana, Umoja wa Ulaya ulitumia zaidi ya $7m (£5.6m) kwa operesheni za WFP nchini Somalia.
Shirika la Marekani la maendeleo ya kimataifa linasema kwa sasa halina mpango wa kusimamisha msaada wa chakula kwa Somalia.