Mabingwa watetezi wa Kombe la mataifa ya Ulaya maarufu kama Euro timu ya Hispania, usiku wa June 21 wamecheza mchezo wao wa tatu wa hatua ya Makundi ya Euro 2016 dhidi ya timu ya taifa ya Croatia na kukubali kipigo cha goli 2-1.
Hispania wamekubali kipigo hicho licha ya wao kuwa wa kwanza kupata goli la uongozi dakika ya 7 kupitia kwa Alvaro Morata dakika ya 5, lakini mambo yalianza kubadilika dakika ya 45 baada ya Nikola Kalinic alipoisawazishia goli Croatia kabla ya kwenda mapumziko, Ivan Perisic ndio aliwatoa vichwa chini Hispania baada ya kufunga goli la ushindi dakika ya 87.
Kipigo hicho kwa Hispania kinahesabika kama cha Croatia kulipa kisasi baada ya mwaka June 18 2012 katika hatua ya Makundi tena Croatia alifungwa goli 1-0 na Hispania, goli pekee ambalo lilifungwa na Jesus Navas dakika ya 89 na kuifanya Croatia kuishia nafasi ya tatu katika hatua ya makundi.
Magoli ya mechi ya Croatia vs Hispania
https://youtu.be/7KaIA5Bx9a8
GOAL AND HIGHLIGHTS: MO BEJAIA VS YANGA JUNE 20 2016, FULL TIME 1-0
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE