Usiku wa November 4 kulichezwa michezo kadhaa ya mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya na tuliona baadhi ya vilabu vikiondoka na point tatu kwa furaha na timu nyingine zikiondoka vichwa chini baada ya kupoteza michezo hiyo, Usiku wa November 5 mechi za UEFA ndogo zilipigwa kama kawaida.
Klabu ya Liverpool ya Uingereza ililazimika kusafiri hadi Urusi kucheza na Rubin Kazan katika muendelezo wa mechi za Kundi B, Liverpool wakiwa ugenini wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0, licha ya kuwa walikuwa ugenini Liverpool walifanikiwa kuibuka na point tatu mbele ya Rubin Kazan.
Hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika hakuna timu iliyokuwa imefanikiwa kuona lango la mpinzani wake, kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kucheza kwa tahadhari, kabla ya dakika ya 52 Liverpool walifanikiwa kupata goli la kwanza kupitia kwa Jordon Ibe, goli ambalo lilidumu kwa dakika zote 90.
Baadhi ya Matokeo ya mechi nyingine za UEFA EUROPA LEAGU November 5
-
Ajax 0 – 0 Fenerbahce
-
Celtic 1 – 2 Molde
-
Sion 1 – 1 Bordeaux
-
Borussia Dortmund 4 – 0 FK Qabala
-
FC Krasnodar 2 – 1 PAOK Thessaloniki FC
-
Club Brugge 1 – 0 Legia Warszawa
-
SSC Napoli 5 – 0 FC Midtjylland
-
Dinamo Minsk 1 – 2 Villarreal
-
Viktoria Plzen 1 – 2 Rapid Wien
Magoli ya Rubin Kazan Vs Liverpool
https://youtu.be/uQ9q4bHpXfE
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.