Everton wamekamilisha usajili wa winga wa Uingereza Jack Harrison kwa mkopo wa msimu mzima kutoka Leeds United.
Aston Villa walichelewa kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 lakini alifuzu vipimo vya afya na Everton siku ya Jumatatu.
Everton ilisema itaendelea na matibabu yake kutokana na jeraha dogo la nyonga kabla ya kuwa tayari kuchaguliwa.
Harrison ni mchezaji wa nne kusajiliwa na Everton majira ya kiangazi kufuatia kuwasili kwa beki wa pembeni Ashley Young, winga Arnaut Danjuma na mshambuliaji Youssef Chermiti.