Usimamizi wa Mradi wa DMDP unafanywa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambapo mpango huu utapita katika Halmashauri za miji mbalimbali Tanzania, miundombinu inayojengwa inatarajiwa kupunguza kero nyingi kama vile mafuriko wakati wa mvua, foleni, na taabu ya usafiri.
Pia itaboresha huduma za kijamii, kupandisha hadhi na kuongeza thamani maeneo yanayopitiwa na mradi huo, hasa katika makazi holela yasiyopimwa na kukuza shughuli za biashara.