Serikali imeanza mkakati wa kutoa chanjo ya mifugo ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kimeta (Anthrax) unaoonekana kuathiri zaidi mifugo na wanyama pori na baadae kuenea kwa binadamu.
Mratibu wa afya kutoka Wizara ya Afya, Juvilet Bernald amesema ugonjwa wa kimeta umekuwa tatizo zaidi kwenye ukanda wa Kaskazini mwa Tanzania ikiwemo Ngorongoro na Monduli ambapo wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakipata maambukizi ya ugonjwa huo kwa kuwa wamekua wakila nyama za mifugo hiyo ikiwa imekufa.
Kwa upande wake Dr. Bedan Masuruli kutoka Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi,ambaye pia ni msajili wa baraza la vetenary,alisema tatizo la kimeta ni kubwa kwa sababu linaathiri pia binadamu na hivyo aliongeza kuwa ipo haja kwa wataalamu kuunganisha nguvu na kutoa elimu kwa maeneo yanayoathiriwa zaidi na ugonjwa huo.
Ulipitwa na hii? Sababu za gharama ujenzi reli ya kisasa awamu ya pili kuwa juu tofauti na ya kwanza