Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dokta Dotto Biteko ameitaka Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuhakikisha wanafikisha huduma ya vituo vya mafuta vijijini Ili kurahisisha upatikana wa Nishati mbadala sambamba na kutoa elimu ya matumizi yake.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dokta James Mataragio kwaniaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Doto wakati uzinduzi wa baraza la wafanyakazi EWURA mkoani Morogoro.
Amesema mpango wa Serikali nikufikia asilimia 80 ya matumizi ya Nishati safi ifikapo mwaka 2034 hivyo wananchi wa vijijini wanatakiwa kusogezewa huduma hizo ili kupunguza matumizi ya Nishati chafu kama mkaa,kuni ambao ndio tegemezi kubwa kwa wakazi hao.
Serikali imesema mpango uliopo maeneo ya vijijini bado yana uhitaji wa vituo vya mafuta na hamasa ya matumizi ya Nishati safi ya kupikia ujenzi wa vituo kupewa kipaumbele ambayo ni agenda ya kupatikana Nishati safi ya kupikia.
Baada ya ufunguzi wa kikao Cha baraza hilo la wafanyakazi wa Ewura, kukafanyika uzinduzi wa Mradi wa Nishati Safi na Salama ya kupikia katika shule ya sekondari ya Morogoro na kambi ya kuelekea wazee ya Fungafunga Morogoro.
Kwa upande Mkurugenzi mkuu wa EWURA Dk James Andilile amesema kuwa Ewura imekuwa ikifanya urejeshaji kwa jamii kila mwaka ambapo kwa shule ya sekondari Morogoro wamefunga majiko na mitungi ya gesi ya kupikia pamoja na Kambi ya wazee Fungafunga.
Andilile amesema kufungwa kwa majiko na mitungi hiyo kutapunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira na kuwa na manufaa makubwa na kwamba matumizi ya gesi yanapunguza muda wa kupikia.
Nao baadhi ya wakazi wa Morogoro wamesema kwa Sasa elimu imekua kubwa ya matumizi ya Nishati safi hivyo wameomba kupunguza bei ya gharama ya gesi na umeme Ili waweze kumudu.