Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA imefanya kikaokazi cha kutambulisha mfumo wa Majis ulioboreshwa kwa ajili ya ukusanyaji wa taarifa kwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira. Kikao hicho kimefanyia EWURA makao makuu Dodoma.
Akifungua kikao hicho kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mha. Poline Msuya amesema Maboresho yaliyofanyika katika mfumo yalichagizwa pia na maoni ya wadau ambao ni watumiaji wa mfumo. Pia mfumo umeboreshwa kuakisi mabadiliko na maendeleo kwenye sekta ya maji.
Aidha EWURA haitosita kuchukua hatua za kiutawala kwa mamlaka za maji ambazo hazitatekeleza uwasilishaji wa taarifa zao kwa wakati, aliongezea Mha. Poline Msuya.
Akitoa maoni yake muwakilishi wa Wizara ya Maji Mha. Epimack Oscar alisisitiza Mamlaka za Maji zitumie mfumo huo kwa ajili ya kuwa na takwimu sahihi.
Kifungu cha 29(1)(h) cha Sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira Sura Namba 272 kinaitaka EWURA kukusanya taarifa za utendaji kutoka mamlaka.