Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji imetangaza ongezeko la bei kwa mafuta yanayoingilia Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kushuka kwa thamani ya Tsh dhidi ya Dola ya Marekani na ongezeko la bei katika soko la Dunia.
Lita moja ya Petroli imepanda kwa Tsh 20 huku Dizeli ikiongezeka kwa Tsh 74 na Mafuta ya taa Tsh 44.
Ikilinganishwa na bei zilizokuwapo Januari 2020, bei za jumla ya Petroli imeongezeka kwa Tsh 20.01 kwa lita, Dizeli imeongezeka Tsh 74.21 na Mafuta ya taa Tsh 43.96 kwa lita moja.
Kanda ya Kaskazini inayopokea mafuta kupitia Bandari ya Tanga nako bei imepanda ambapo bei ya rejareja ya Petroli imeongezeka kwa Tsh 42 kwa lita wakati Mafuta ya taa yakipanda kwa Tsh 2 lakini Dizeli ikishuka kwa Tsh 18.
Bei ya jumla ya Petroli imeongezeka kwa Tsh 41.94 na Mafuta ya taa kwa Tsh 2.37 kwa kila lita moja ikilinganishwa na bei za Januari huku dizeli ikishuka kwa Tsh 17.49.
Kanda ya Kusini inayojumuisha Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma bei za rejareja ya Petroli imepanda kwa Tsh 35 wakati Dizeli ikishuka kwa Tsh 22. Ikilinganishwa na Januari, bei ya jumla ya Petroli imepanda kwa Tsh 35.27 kwa lita.