Aliyekuwa mpenzi wa mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei, ambaye anadaiwa kumuua kwa kumwagia petroli na kumchoma moto, amefariki kutokana na kuungua wakati wa shambulio hilo, hospitali ya Kenya alikokuwa akitibiwa ilisema Jumanne.
Cheptegei, 33, ambaye alishiriki katika mbio za marathon katika Michezo ya Olimpiki ya Paris, aliungua hadi zaidi ya 75% ya mwili wake katika shambulio la Septemba 1 na alikufa siku nne baadaye.
Mpenzi wake wa zamani, Dickson Ndiema Marangach, alifariki saa 7.50 usiku kwa saa za nyumbani Jumatatu, alisema Daniel Lang’at, msemaji katika Hospitali ya Kufundisha na Rufaa ya Moi huko Eldoret magharibi mwa Kenya, ambapo Cheptegei pia alitibiwa na kufariki.
“Alikufa kutokana na majeraha yake, majeraha ya moto aliyopata,” Lang’at aliambia Reuters.