Mwanamitindo Kasia Lenhardt (25) ambaye alikuwa mpenzi wa mchezaji wa FC Bayen Munich Jerome Boateng amekutwa kafariki katika apartment yake jana mjini Berlin nchini Ujerumani.
Kifo cha Kasia kimetokea ikiwa ni wiki moja imepita toka wawili hao waachane lakini kifo chake Polisi bado hawajakihusisha au kumshuku yeyote licha ya wawili hao kuachana kwa ugomvi ambao ulienda hadi katika mitandao ya kijamii.
Kasia ambaye alikuwa na mahusiano na Boateng kwa miezi 15 ameacha mtoto mmoja ambaye alimpata katika mahusiano yake yaliopita kabla ya kuwa na Boateng.