Haijalishi umeipata kwa style gani ili mradi tu njia unayoitumia kuitafuta iwe halali na imethibishwa kwenye viwango vyote vya matumizi ya fedha halali ya Kitanzania, kama ilivyo siku zote maisha ni safari tena yenye fumbo kubwa ndani yake, mwanzo ni mgumu ila huwenda ukalia kivulini kama uvumilivu na subra itavipa kipaumbele, leo hii ungewezaje kufahamu Michael Kenedy wengi tumemfahamu kama Afande Mura ambae umaarufu wa jina lake umekuja baada ya Styyle yake ya Uchezaji kwenye maeneo tofauti ikiwemo sehemu za starehe…aah huyu jamaa ni mkali wa kucheza amapiano ni balaa na nusu.
Lakini historia yake haikuanza jana, unaambiwa amewahi kukataliwa hadi na Mama yake mzazi kisa tu kutaka kuishi Dar es salaam, kosa alilolifanya ni kutoroka Mbeya alipokuwa akiishi na Baba yake, baada ya Mama yake kumuacha kwa Mzee wake, lakini hakutaka iwe hivyo.
Huwezi amini kumbe hata Dar amekuja kwa lift ya gari la mizigo, sehemu yake ya kwanza kuikanyaga ardhi ya Dar es salaam ilikuwa ni Ubungo terminal, Michael alipafanya stand kuwa makazi yake ya kudumu kwa siku tatu, kila ulipofika usiku alitandika box chini na kulala wakiwa hafahamu ni wapi ataelekea, akiwa bado kwenye harakati za kutafakari ni wapi aanzie maisha, alikutana na Mjomba wake bila kutarajia ambae alimchukua na kumpeleka nyumbani kwa Mama yake Mbagala, kilichofata ni kichapo kwanini atoroke kwa Mzee wake Mbeya?
Michael alishindwa kuvumilia viboko vya kila asubihi na kuamua kuondoka nyumbani, ndipo rasmi msoto wa maisha ya Dar es salaam ukaanza upya.
KWA STORI ZAIDI UNAWEZA UKABONYEZA PLAY KUFAHAMU ZAIDI.