Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa hapa nchini miongoni mwa Ma-RC wapya yumo Queen Sendiga ambaye aligombea urais kwa tiketi ya chama cha ADC katika uchaguzi mkuu wa 2020 ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
AyoTV na millardayo.com imefanya mahojiano na Queen Cuthbert Sendiga ili kufahamu yeye amepokeaje taarifa za kuteuliwa kwake na ipi itakuwa mipango yake lakini pia kufahamu kama atarudi CCM baada ya kuteuliwa.
“Taarifa nilipata nikiwa nyumbani kama Mama nina majukumu mengi ya familia, nilishangaa niliposhika simu nilikuta simu nyingi, meseji nyingi, nikathibitisha kuteuliwa kupitia taarifa iliyotolewa kwa umma na Ikulu” Queen
“Mkoa wa Iringa nilipita wakati nafanya kampeni, watu wa Iringa wategemee wanampata mwana Iringa mwingine naenda kuwa mmoja ya wanafamilia ya Iringa, tunaenda kuendeleza mazuri yaliyofanywa na aliekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, nitacheza ngoma inayopigwa Iringa, kwa hiyo nitakwenda kulingana na watu wa Iringa kutatua changamoto zilizopo” Queen
“Watu wa Iringa pia wategemee ushirikiano wa 100% kuhakikisha kwamba tunaisogeza Iringa iwe bora zaidi, Siasa zina vitu vingi zile fujo zilipita na sasa ni maisha mapya, Mimi lile lilimalizika siku ileile nilipokuwa Iringa na kesho yake nilifanya mkutano Iringa” Queen