Wakati Dunia ikipanga kuwa kufikia mwaka 2030, kuna patikana usawa wa kijinsia katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo maeneo mengi Duniani ikiwemo Tanzania, Wanawake nao wameanza kujiinua wenyewe kwa kuziendea fursa, hali hii haiendi mbali na juhudi za Stella Elias ambae licha ya kuwa Mama wa watoto wanne anaeyaendesha maisha yake kwa kupitia kazi ya ufundi simu.
Histori ya maisha ya Stella haikuwahi kuwa rahisi hata kidogo hadi hali leo hii kuupata ujuzi wa kutekengeza simu, Kwani hana Baba na Mama, wala ndugu yeyote kwa pande zote mbili za Wazazi wake, kitu kina muumiza Stella ni hakuwahi kumuona Baba yake, hakuwahi kuwa na kumbukumbu nzuri ya kifo cha Mama yake…..
Akiwa na umri wa kuanza shule Stella alichukuliwa kuwa msaidizi wa kazi za ndani, baada ya kuletwa Mwanza na majirani zake mwaka 1994, mwaka mmoja baadae alipata mwanaume aliyemrubuni atoroke kurudi kwao Bukoba ili amuoe na kweli Stella alifanya hivyo kwa mapenzi na walifanikiwa kuoana na kupata watoto wawili
Stella amefunguka mengi kwenye Interview ya maisha yake, kutoka kuwa Mfanyakazi wa ndani hadi kuwa fundi simu.