Ni siku chache zimepita tangu yalipofanyika Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani March 08,2024 ambapo Dunia imeitumia siku hiyo kutambua michango ya Malkia wa na Wanawake Wapambanaji wanaotumia akili, ubunifu na vipaji walivyonavyo kufanya mambo makubwa na kubadilisha fikra, mitazamo na hata kukuza uchumi kwenye Jamii.
Leo nakukutanisha na Catherine Shembilu Malkia wa Nguvu kutoka Mkoani Tanga ambaye baada ya kuhitimu Chuo Mkoani Iringa aliiona fursa ya kuviongezea thamani vikapu na kuvifanya vyenye ubora utakaowezesha viuzwe kwa bei ya juu ndani na nje ya Nchi na kuwakomboa Wanawake.
Akiwa ameanza na Mtaji wa Tsh. Milioni 1 tu aliianzisha safari yake na sasa Catherine ni Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Vikapu Bomba ambayo inafanya kazi na Wanawake wa Vijijini zaidi ya 300 wa Mikoa ya Iringa na Njombe kwa kuwawezesha kutengeneza bomba vya kisasa na kuwatafutia masoko ndani na nje ya Nchi ambayo yanaanya wauze kwa bei kubwa nzuri inayowafanya waepukane na umasikini.
Tazama zaidi…