Kutokana na tatizo la hofu ya usalama Kenya leo tulisikia ishu ya walimu kugoma kwenda kufanya kazi maeneo ya kaskazini mwa Kenya.. kingine ilikuwa ishu ya wahudumu wa afya pia kukimbia maeneo hayo kutokana na hofu ya mashambulizi hayo pia.
Kaskazini mwa Kenya hali sio shwari sana, hii story inatoka maeneo ya Turkana ambako Afisa mmoja wa Polisi Alfred Lokori amelazimika kuchukua jukumu la kuwahudumia wenyeji wa eneo hilo katika kituo cha Afya cha Lomelo, kituo hicho hakina wahudumu kabisa.
“sasa nimekuwa Askari mahali pengine na mahali pengine nimekuwa ni daktari “; Alfred Lokori.
Tukio kama hili liliripotiwa wiki iliyopita katika kaunti hiyohiyo ya Turkana ambako kijana mmoja alijitokeza kufanya kazi ya udaktari ambayo haifahamu kutokana na ukosefu wa wahudumu wa Afya katika eneo hilokutokana na kukosekana kwa usalama.
Nimekuwekea taarifa hiyo iliyoripotiwa na kituo vha K24 kuitazama bonyeza play hapa chini..
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenyeTwitter,Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa>>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribeYouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.