Nchini India kuna utamaduni wa mwanamke kutoa mahari kwa familia ya mwanaume anayetaka kuolewa naye. Japokuwa utamaduni huo ni kinyume na sheria nchini humo tangu 1961 bado kuna watu wanauendeleza.
Taarifa za hivi karibuni ni kwamba, Jeshi la Polisi katika Jimbo la Kaskazini la Uttarakhand linamshikilia mwanamke mmoja ambaye amedanganya kuwa mwanaume tangu mwaka 2014 ili alipwe mahari.
Binti huyo aliyetambuliwa kwa jina la Krishna Sen mwenye miaka 26, anaripotiwa kufunga ndoa mwaka 2014 na mwanamke mwenzie baada ya kulipwa mahari lakini cha kushangaza ni kwamba mara tu baada ya harusi hiyo, wawili hao waliachana.
Inaelezwa pia kuwa Krishna ‘alioa’ kwa mara ya pili mwaka 2017 na kulipwa tena mahari, lakini shemeji zake wamekuwa wakilalamika na tayari wamemshtaki kwa vitendo vyake vya kumnyanyasa dada yao ikiwa ni pamoja na kuomba wampe pesa afanyie biashara kwa ahadi ya kuzirudisha lakini hajawahi kuzirudisha.
Maafisa wa polisi wameeleza kuwa Krishna aliwaambia kwamba amekuwa akitaka kuwa mwanaume na kuishi kama mume lakini hata hivyo haijulikani kama wazazi wake wanafahamu anayofanya binti yao.
Polepole, Lukuvi na Musukuma kwenye kufunga Kampeni za CCM Siha