Kesi inayomkabili Isaac Abakuk ambaye anatuhumiwa kumtukana Rais John Magufuli kwenye ukurasa wake wa facebook June 08 2016 imeshindwa kuendelea kutokana na upande wa Jamhuri kutokamilisha ushahidi na kuiomba Mahakama kuahirisha shauri hilo hadi kesho June 08 2016.
Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Augustine Rwezire wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha amekubali ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo ambapo inatarajiwa kuanza kusikilizwa mfululizo, mshtakiwa anaendelea kuwa nje kwa dhamana kusubiri kesi yake itakapotajwa.
Kesi ya aliyemtukana Rais Magufuli facebook imeshindwa kuendelea kutokana na Jamhuri kutokamilisha ushahidi, Kesi itaanza kusikilizwa kesho
— millardayo (@millardayo) June 7, 2016
ULIKOSA HII YA ALIYEMTUKANA RAIS MAGUFULI FACEBOOK KUFIKISHWA MAHAKAMANI ARUSHA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE