June 08 2016 Mahakama Kuu kanda ya Arusha ilitoa maamuzi kwa Isaac Abakuk ambaye alishitakiwa kwa kumtukana Rais John Magufuli kwenye ukurasa wake wa facebook ambapo mshitakiwa alitakiwa kulipa millioni 7 au kutumikia kifungo cha miaka 3 gerezani.
Baada ya kukiri kukiri kutenda kosa hilo mahakama iliamuru alipe fedha hizo kwa awamu mbili, katika awamu ya kwanza atalipa July 8 2016 sh mil 3.5 na August 8 2016 atalipa kiasi kilichobaki cha sh mil 3.5.
Leo June 17 2016 amekabidhiwa kitita cha shilingi milioni 4.5 kama sehemu ya kwenda kulipa faini mahakamani, fedha hizo zilichangwa na wanaharakati na wadau wa mitandao kupitia mratibu wa ukusanyaji wa michango hiyo kwa kanda ya kaskazini Ephata Nanyaro.
Aliyemtukana Rais Magufuli Facebook amekabidhiwa mil 4.5 ili kulipa faini mahakamani baada ya wadau kumchangia pic.twitter.com/vvvaVdJ9C2
— millardayo (@millardayo) June 17, 2016
ULIKOSA HII YA ALIYEMTUKANA RAIS MAGUFULI FACEBOOK KUFIKISHWA MAHAKAMANI? BONYEZA PLAY HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE