Zaidi ya Wafanyakazi 200 wa Facebook wamedai Kampuni hiyo inawalazimisha wasimamia maudhui kurudi ofisini licha ya hatari ya kupata maambukizi ya Corona Virus.
Wafanyakazi hao wanadai Kampuni hiyo inahatarisha maisha ili kupata faida huku wakitaka ifanye mabadiliko kuruhusu kazi kufanyika nje ya Ofisi na vilevile kutoa manufaa mengine.
Akijibu madai hayo, Msemaji wa Facebook amesema idadi kubwa ya wasimamia maudhui 15,000 wamekuwa wakifanya kazi nyumbani na wataendelea kufanya hivyo.
Mwezi August mwaka huu, Facebook ilitangaza kuwa wafanyakazi wake watafanya kazi kutokea nyumbani hadi 2021.