Fadhili Fabian Ngajilo ambaye ni Mdhamini mkuu wa ligi ya inayojulikana kama ‘NGAJILO MUNICIPAL LEAGUE 2024’ amekabidhi vifaa vya michezo ikiwemo mipira na jezi vitakavyotumika kwenye ligi hiyo ambapo jumla ya timu 16 za mpira wa miguu katika Manispaa ya Iringa zimethibitisha kushiriki Ligi hiyo vilivyo anza kutimua vumbi leo Julai 16, 2024 huku lengo kuu likiwa ni kutoa fursa kwa vijana kuonyesha vipaji walivyonavyo, kuchangamsha mkoa na kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vinavypoatikana katika mkoa wa Iringa.
Akizungumza wakati wa ziezi la kugawa vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu shiriki tukio lililofanyika Katika uwanja wa CCM Samora uliopo Manispaa ya Iringa Mdhamini mkuu wa ‘Ngajilo Municipal League 2024’, Fadhili Fabian Ngajilo, amesema maandalizi yamekamilika na matarajio ya Ligi hiyo ni kusaidia juhudi za Serikali kwenye kuzalisha ajila na kutangaza utalii.
“Lengo la ligi hii ni kuchangamsha mkoa kiburudani na kiutalii, Binafsi nafurahi kudhamini ligi hii na sisi kama Vunjabei Company, furaha yetu ni kuona vijana wa Iringa wanapata fursa ya kushiriki michezo ambayo ina fursa nyingi za ajira lakini pia kuwatoa vijana katika makundi hatarishi” – Amesema Ngajilo
Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu wilaya ya Iringa, Yahya Mpelembwa, amesisitiza vilabu vyote vitakavyoshiriki michuano hiyo kuhakikisha vifaa vilivyoletewa vinaenda kutumika kama ilivyopangwa.
“Tunatamani kuona vifaa hivi vinaenda kutumika kama tulivyopanga na kuwa chachu ya maendeleo ya soka katika maeneo yetu” – amesema Mpelembwa.