Leo Novemba 12, 2020, katika Mkutano wa tatu wa Bunge la 12, Waziri Mkuu wa Serikali itakayoongoza 2020 hadi 2025 atafahamika rasmi kwa mchakato unakuwa kama ifuatavyo.
Spika wa Bunge atapokea barua kutoka kwa Rais yenye jina la mteule wa nafasi hiyo, atasoma ujumbe uliomo ambao utakuwa umeambatana na jina la Waziri Mkuu aliyeteuliwa na Rais.
Kisha Spika ataahirisha Bunge kwa dakika 45 ili kuwapa nafasi wabunge kutafakari uteuzi huo kisha kumthibitisha.
Rais Magufuli amesema ana uwanda mpana wa kuchagua mawaziri kutokana na kuwa na wabunge wengi wa CCM tofauti na muhula ulipita.
Via JF