Familia za Waisraeli waliotekwa na Hamas walijaribu kuzuia kuingia kwa msaada wa kibinadamu katika Ukanda wa Gaza siku ya Jumanne, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.
Polisi wa Israel walizuia maandamano ya familia za mateka ambao walikuwa na nia ya kufunga kivuko cha Kerem Shalom wakipinga kupelekwa kwa shehena za misaada katika eneo hilo, gazeti la Haaretz liliripoti.
Familia hizo zinataka kuachiliwa kwa makumi ya mateka wa Israel wanaoshikiliwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza kufuatia shambulio lake la kuvuka mpaka tarehe 7 Oktoba.
Takriban Waisrael 136 wanaaminika kushikiliwa na kundi la Wapalestina.
Israel imeshambulia Ukanda wa Gaza tangu shambulio la Hamas, na kuua Wapalestina wasiopungua 23,210, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kuwajeruhi wengine 59,167, kulingana na mamlaka ya afya ya eneo hilo.
Takriban Waisrael 1,200 wanaaminika kuuawa katika mashambulizi ya Hamas.
Takriban 85% ya watu wa Gaza wameyakimbia makazi yao, huku wote wakiwa hawana chakula, kulingana na Umoja wa Mataifa. Mamia ya maelfu ya watu wanaishi bila makao, na chini ya nusu ya malori ya misaada yanaingia katika eneo hilo kuliko kabla ya vita kuanza.