Kila asubuhi Millard Ayo atazisogeza karibu yako habari zote kubwa kutoka kwenye Magazeti mbalimbali ya Tanzania ambapo huwa naziweka kwenye page ya Twitter ya @millardayo na kwenye Youtube ya millardayo bila kusahau millardayo.com.
Hizi hapa chini ni zile kubwa kutoka kwenye Magazeti ya Tanzania leo December 31 2016 ambapo mojawapo ni kutoka gazeti la Nipashe kuhusu sakata la faru John ambapo serikali imezuia utoaji wa taarifa holela zinazotolewa na watu mbalimbali na kusisitiza kuwa mwenye kuidhinisha jambo hilo siyo mtu mwingine isipokuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
#NIPASHE Serikali imesema taarifa za faru John kwa umma hazipaswi kutolewa kiholela na mtu yeyote bali zitoke kwa waziri mkuu pic.twitter.com/4O9gii5Hx2
— millardayo (@millardayo) December 31, 2016
#NIPASHE Matukio ya ubakaji na ulawiti yamekuwa kinara ktk jiji la DSM kuanzia mwezi January hadi December mwaka huu pic.twitter.com/0FLmglbkB0
— millardayo (@millardayo) December 31, 2016
#NIPASHE Kasi kufungwa maduka tishio, 1,800 yatoweka kwa miezi mitano Dar, Arusha, Waziri Mpango asema bado haijafahamika ni kwa nini pic.twitter.com/T3GZhzwENY
— millardayo (@millardayo) December 31, 2016
#NIPASHE Bei mpya ya umeme yenye ongezeko la 8.5% kwa uniti, imeibua hofu ya kuongezeka kwa gharama ktk huduma na bidhaa mbalimbali pic.twitter.com/JwS2d6CYJc
— millardayo (@millardayo) December 31, 2016
#NIPASHE Halmashari ya K'ndoni imetia saini mkataba na kampuni ya ujenzi ya Estim kwa ajili ya kujenga barabara 5 ambazo zitagharimu bil 22 pic.twitter.com/J9kVGcT8NH
— millardayo (@millardayo) December 31, 2016
#MWANANCHI Wasomi wabainisha yanayotakiwa yasijirudie 2017
1.Bunge 'gizani'
2.Matamko
3.Migogoro ya ardhi
4.Amri ya kuzuia siasa majukwaani pic.twitter.com/QSkpBc9M5u
— millardayo (@millardayo) December 31, 2016
#MWANANCHI Suala la ugumu wa maisha linatajwa kuwa moja ya mambo yaliyowatikisa wananchi ktk mikoa mbalimbali kwa mwaka 2016 pic.twitter.com/NclAAqMCXd
— millardayo (@millardayo) December 31, 2016
#MWANANCHI Rais kuteua jaji mkuu mpya au kumwongezea muda Jaji Chande baada ya leo kufikia ukomo wa umri wa kutumikia nafasi hiyo kikatiba pic.twitter.com/9mbvpXTbI9
— millardayo (@millardayo) December 31, 2016
#MWANANCHI Ikiwa ni miezi minane tangu Rais Magufuli aahidi kuonyeaha hati ya malipo ya mshahara wake, Zitto amemtaka kutekeleza ahadi hiyo pic.twitter.com/b0ZESFGQSi
— millardayo (@millardayo) December 31, 2016
#MWANANCHI Utajiri wa bilionea namba moja Afrika, Dangote umeporomoka kwa theluthi moja 2016 na kumshusha kwenye orodha ya matajiri duniani pic.twitter.com/n2K7OFTmUC
— millardayo (@millardayo) December 31, 2016
#MWANANCHI Mwanafunzi chuo kikuu huria TZ atupwa jela miaka 30 kwa kulawiti alimtongoza mvulana '16' wa shule ya sekondari kupitia facebook pic.twitter.com/h8cZ0OOGal
— millardayo (@millardayo) December 31, 2016
#MWANANCHI Hayatasaulika 2016
Mateke ya Koffi Olomide
Chura wa Snura
Maji ya Ray
Bifu la Dimpoz na Diamond
Zengwe la Ali Kiba na MTV Ema pic.twitter.com/vOiuZEMWxK
— millardayo (@millardayo) December 31, 2016
#MTANZANIA Waziri Mpango amesema hakuna mdodoro wa uchumi, ashangazwa na biashara kufungwa Dar na Arusha pic.twitter.com/azPN8BzhRQ
— millardayo (@millardayo) December 31, 2016
#MAJIRA Shanghai Shenhua yatangaza kuwa wameshakamilisha usajili wa Carlos Tevez kwa ajili ya kukitumikia kikosi chao ktk ligi kuu ya China pic.twitter.com/7JaJeJBVEu
— millardayo (@millardayo) December 31, 2016
#HabariLEO Imeelezwa kuwa hospitali ya wilaya ya Sikonge Tabora inakabiliwa na tatizo sugu la kunguni, hivyo kuhatarisha afya za wagonjwa pic.twitter.com/RdviZGJXgW
— millardayo (@millardayo) December 31, 2016
#TanzaniaDAIMA 80% ya wazazi mijini hawana muda wa kuzungumza na watoto wao hali inayosababisha kuporomoka kwa maadili kwa watoto hao pic.twitter.com/WfuZ0hMpI4
— millardayo (@millardayo) December 31, 2016
#HabariLEO Serikali kupitia kitengo cha uchunguzi wa jinai ya kimtandao kimewakamata watuhumiwa 690 kwa tuhuma za kufanya uhalifu wa mtandao pic.twitter.com/CnbLHikTpE
— millardayo (@millardayo) December 31, 2016
AyoTVMAGAZETI: Kasi ya kufungwa maduka tishio, Hofu yatanda bei mpya ya umeme, Bonyeza play hapa chini