Leo July 27, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia kwa dhamana Mbunge Tundu Lissu baada ya kutimiza masharti kwa kuwa na wadhamini wawili wenye bondi ya Tsh. Milioni 10 kila mmoja huku akipewa sharti la kutotka nje ya nje ya Dar es Salaam.
Kesi yake imeahirishwa hadi August 24 ambapo nje ya Mahakama hiyo Wakili anayeongoza jopo la Mawakili 18 wanaomtetea Tundu Lissu, Fatma Karume amezungumza na kusema:>>>”Kwenye hili shujaa ni mmoja. Sio Wanasheria, Shujaa ni mtu mmoja tu Tundu Lissu. Alikuwa tayari kukaa ndani hata wiki moja kutetea haki yake ya uhuru wa kuongea.” – Fatma Karume.
ULIPITWA? Polisi walivyomzuia Wakili wa Tundu Lissu, Fatma Karume kuzungumza…tazama kwenye video hii!!!