Kila asubuhi Millard Ayo atazisogeza karibu yako habari zote kubwa kutoka kwenye Magazeti mbalimbali ya Tanzania ambapo huwa naziweka kwenye page ya Twitter ya @millardayo na kwenye Youtube ya millardayo bila kusahau millardayo.com.
Hizi hapa chini ni zile kubwa kutoka kwenye Magazeti ya Tanzania leo January 02 2017 ambapo mojawapo ni kutoka gazeti la Nipashe kuhusu Zitto Kabwe kuzungumzia utumbuaji majipu wa serikali ya awamu ya tano kwa kusema kuwa nguvu kubwa imeeleekezwa katika kutumbua na kusahau kuboresha maisha ya Watanzania.
#HabariLEO Kilichomponza bosi TANESCO
1.Kupandisha bei ya umeme bila kumshirikisha waziri
2. Kuwakamua maskini fedha na kujilipa bonasi pic.twitter.com/8VfLuImtPd
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#JamboLEO Askofu Josephat Gwajima amesema amekuwa na maono ya kumiliki treni ya abiria kutoka Dar es salaam kwenda Mwanza pic.twitter.com/GZGswoMmn3
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#JamboLEO Manispaa ya Kigamboni DSM kubadilisha mfumo wa mji kutoka kwenye uvuvi hadi utalii baada ya kubainika mji huo una vivutio vingi pic.twitter.com/GqHjw7v8qk
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#JamboLEO Chuo cha kikatoliki Mwenge K'njaro, kimeanzisha kozi ya ujasiriamali kwa wanafunzi wake kikiwa na lengo la kuwawezesha kujiajiri pic.twitter.com/deDMS2C34r
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#MTANZANIA Lowassa apongeza raia wa Marekani kwa kumchagua Trump kuwa Rais mpya wa nchi hiyo, asema atakuwa Rais mwenye kufanya uamuzi mgumu pic.twitter.com/hIlGfpbFyC
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#MTANZANIA Manispaa ya Ilala DSM inahitaji zaidi ya bil 3 ili kubadili miundombinu ya machinjio ya Vingunguti yaweze kuwa ya kisasa pic.twitter.com/88M5CQ7cVG
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#MTANZANIA 'TANESCO imezidiwa na madeni haina ujanja mwingine':- David Kafulila pic.twitter.com/DLlJiMXqiV
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#MTANZANIA Baada ya Serikali kutangaza kusitisha utoaji wa mikopo wanafunzi wanaosoma China, wanafunzi wamemuomba Rais kutengua uamuzi huo pic.twitter.com/o17XziPowT
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#MTANZANIA Watoto 27 wamezaliwa usiku wa mkesha wa sikukuu ya mwaka mpya 2017 ktk hospitali mbalimbali DSM, kati yao wa kiume 16, wa kike 11 pic.twitter.com/tjrpic86dZ
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#MTANZANIA Wadudu aina ya kupe wametajwa kuwa chanzo cha ng'ombe kukosa maziwa na kusababisha bei ya maziwa kupanda maradufu Misenyi Kagera pic.twitter.com/hMGlDHoLSF
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#MTANZANIA 39 wakiwamo wageni 16 wamekufa kufuatia mashambulizi ya 'kigaidi' Uturuki baada ya mtu kuwamiminia risasi kwenye klabu ya usiku pic.twitter.com/C8HQzOExcd
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#TanzaniaDAIMA Imeelezwa kinga ya pepopunda imeadimika ktk baadhi ya hospitali kubwa DSM hali iliyozua hofu kwa wananchi hasa wajawazito pic.twitter.com/mlmpqPlkwY
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#TanzaniaDAIMA Mkulima Omary ashambuliwa na kujeruhiwa vibaya kwa kukatwa na panga kichwani na mfugaji kijiji cha mamoyo Mikumi Morogoro pic.twitter.com/xp9VnHCevU
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#NIPASHE RC Mbeya, Makalla awapa siku 7 machinga wanaofanya ovyo biashara mitaani, kuondoka na kuingia nazo ndani ya soko la Mwanjelwa pic.twitter.com/ZMS2RCZxvg
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#NIPASHE Serikali iko ktk mazungumzo ya kupata teknolojia mpya itakayosaidia upatikanaji wa nyumba za bei nafuu kwa wenye kipato cha chini pic.twitter.com/EuLaeTGvi8
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#MTANZANIA Serikali Singida inatarajia kujenga kiwanja kikubwa cha ndege kitakachowezesha ndege kubwa za abiria na mizigo kutua pic.twitter.com/jvb8Np9PDH
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#MWANANCHI Mahakama kuu imemwondolea DPP mamlaka ya kutoa adhabu isiyokatiwa rufaa kwa mshtakiwa anayekiri makosa ya kimtandao pic.twitter.com/Hy2sCrZ4k8
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#MWANANCHI Mzee wa upako aendelea kuwashambulia wanahabari na jana amesema hawatamshinda kwa vita ya maneno labda watumie risasi pic.twitter.com/NZF3qIpWhP
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#MWANANCHI Utoro wawapotezea ajira watumishi watatu Mbulu, mkurugenzi Hudson Kamoga asema uamuzi huo uwe funzo kwa watumishi wengine wa umma pic.twitter.com/ojY9xyKPj7
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#MWANANCHI Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amewataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii badala ya kutegemea misaada pic.twitter.com/YSgwFnkBue
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#MWANANCHI Malori ya mafuta yajazana mpakani Zambia, inadaiwa ni kutokana na nchi hiyo kudhibiti ukaguzi wa ushuru kwa bidhaa zinazotoka TZ pic.twitter.com/5sggvk2lnm
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#MWANANCHI Serikali kujenga kuta kukabiliana na mawimbi ya bahari ya hindi yanayosababisha uharibifu wa fukwe Dar es salaam pic.twitter.com/OUdVtVFyse
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#MWANANCHI Mtoto mwaka mmoja Bukombe afariki dunia baada ya kutumbukia kisimani wakati akicheza na wenzake nyumbani kwa mama yake mdogo pic.twitter.com/xfdGS5BWRL
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#MWANANCHI Naibu Waziri Mabula ameyalaumu mabaraza ya ardhi akisema yamekuwa kichocheo cha migogoro kutokana na wajumbe kutokuwa na uelewa pic.twitter.com/X7g2WUkiUI
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
#MWANANCHI TASAF imeziondoa kaya 704 ktk mpango wa kunusuru kaya maskini mkoani Arusha baada ya kubainika hazina sifa pic.twitter.com/0N7xzkGqRg
— millardayo (@millardayo) January 2, 2017
AyoTVMAGAZETI: Vigogo Escrow waipa mtihani Korti Mafisadi, Kilichomponza bosi Tanesco, Bonyeza play hapa chini
unazitaka Breaking NEWS na Stori zote? ungana na Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyeza hapa >>> FB Twitter Instagram YouTUBE