Kiungo wa kimataifa wa Hispania anayeichezea klabu ya Chelsea ya Uingereza Cesc Fabregas amefunguka na kueleza lililomfanya kocha wa zamani wa klabu ya hiyo Jose Mourinho atimuliwa kazi mwezi December, licha ya kuipatia Ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita.
Fabregas ameweka wazi wakati akifanya mahojiano na kituo cha tv cha Sky Sports kuwa, bado anawasiliana na kocha wake wa zamani wa Chelsea na siku zote huwa anawalaumu wachezaji wa Chelsea kwa kumuangusha na kusababisha apoteze ajira yake Stamford Bridge.

“Na muheshimu sana Mourinho na bado huwa tunawasiliana, kosa lake kubwa alilolifanya Chelsea ni kutuamini kupita kiasi na kutupa mapumziko ya mara kwa mara, kwa sababu tulikuwa mabingwa, hiyo ndio sababu iliyomfanya aondoke” >>> Cesc Fabregas
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
KAMA ULIIKOSA VIDEO YA MAGOLI YA SIMBA VS COASTAL UNION APRIL 17 2016, FULL TIME 1-2