Mapenzi ya wachezaji katika vilabu fulani barani Ulaya, imekuwa kawaida hata kama hawavichezei. December 28 klabu ya FC Barcelona imeingia kwenye headlines baada ya kumsainisha mchezaji na kisha kufuta mkataba wake masaa machache baada ya kugundua kuwa ametweet vitu ambavyo vinaihusu timu ya Real Madrid.
Baada ya kufuzu majaribio na Barcelona B Sergi Guardiola alisaini mkataba lakini ulifutwa mapema, baada ya mashabiki wa klabu hiyo kufanya jitihada za kufuatilia mtandao wake wa twitter na kuona posts ambazo zinaonesha mapenzi na Real Madrid.
Hii si mara ya kwanza kwa tukio kama hili kutokea. July mwaka huu klabu ya Depotivo de la Coruna iliwahi kuvunja mkataba na mchezaji Julio Rey baada ya kugundua kuwa aliwahi kutweet vitu ambavyo haviendani na timu hiyo.
Hii ndio Statement ya FC Barcelona
“FC Barcelona imetangaza kuamua kuvunja mkataba na Sergi Guardiola ambaye angejumuisha katika kikosi cha Barcelona B, baada kugundua kuwa aliwahi kutweet post ambazo ni kinyume na Barcelona”
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.