Michezo ya robo fainali ya michuano ya klabu Bingwa Barani Ulaya ilichezwa usiku wa April 5 2016 katika viwanja vya Nou Camp ulizikutanisha timu za FC Barcelona dhidi ya Atletico Madrid na katika uwanja wa Alianz Arena ulichezwa mchezo wa FC Bayern dhidi ya Benfica.
Mchezo wa FC Barcelona dhidi ya Atletico Madrid unatajwa kupata watazamaji wengi zaidi, kwani ulikuwa unazikutanisha timu zinazofuatana katika Ligi, ila FC Barcelona wengi walitaka kuona watakubali kupoteza mchezo leo kwa mara ya pili mfululizo, baada ya rekodi yao ya kutofungwa toka October 3 2015 kuvunjwa na Real Madrid weekend iliyoisha.
FC Barcelona hawakuwa tayari kuona wakiweka rekodi ya kufungwa kwa mara ya pili mfululizo katika uwanja wao wa nyumbani, licha ya kuwa walianza kufungwa goli dakika ya 25 na Fernando Torres, ila Luis Suarez ndio akaiokoa FC Barcelona kwa kufunga magoli mawili dakika ya 63 na 74 na kuendeleza rekodi ya kufunga jumla ya goli 8 katika mechi 8.
Kazi imebakia kwa klabu ya Atletico Madrid April 13 kuisubiri FC Barcelona katika mchezo wao wa marudiano ambao ndio mchezo utakaoamua nani afuzu kucheza nusu fainali ya michuano ya klabu Bingwa Ulaya msimu wa 2015 /2016. Kwa upande wa FC Bayern wao wameibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Benfica.
Video ya magoli ya mchezo wa FC Barcelona Vs Atletico Madrid
https://youtu.be/XOXpi2CJzVo
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ULIIKOSA VIDEO YA MAGOLI YA YANGA VS NDANDA FC FA CUP 2016? HII HAPA