Kutoka nchini Australia leo February 15, 2018 Waziri Mkuu wa nchini hiyo Malcolm Turnbull ametangaza hadharani kupitia mkutano wa waandishi wa habari kuwa atakataza Mawaziri wote wa nchi hiyo kutokuwa na mahusiano ya kimapenzi na wafanyakazi walio katika ofisi moja.
Ameeleza hivyo alipoitisha mkutano huo wa waandishi wa habari ili kuwaambia kuwa Naibu Waziri Mkuu Barnaby Joyce alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mfanyakazi wa zamani wa ofisi hiyo jambo ambalo amesema halikubaliki.
Turnbull amemsimamisha kazi kwa muda Barnaby kutokana na kilichotokea kupisha kikao cha kufanya uchunguzi na kuamua kama alichokifanya Barnaby ni sawa ama lah ili kwamba waamue cha kufanya.
Ukarabati uliogharimu Milioni 75 wamfanya Ndalichako kuchukua maamuzi Magumu
DPP kutoa uamuzi kuhusu Mhasibu wa TAKUKURU