Kwa watu na sababu nyingi mbalimbali inaaminika kuwa chooni ndiyo sehemu yenye vimelea na uchafu mwingi ambao huweza kusababisha maambukizi ya magonjwa.
Hata hivyo utafiti wa watu mbalimbali unaonesha vitu 5 ambavyo huwa vichafu zaidi ya kiti cha choo (cha kukaa au kuchuchumaa) cha nyumbani kwako. Vitu hivyo ni kama vilivyotajwa hapa chini.
1. Zulia (Carpet)
Hii ni namba moja ambapo inaelezwa kuwa japokuwa zulia hupendezesha nyumba na huleta muonekano wa usafi nyumbani, utafit unaonesha kuwa zulia lako hili la ndani huwa na bakteria 700 zaidi ya waliopo kwenye kiti cha chooni kwako.
Bakteria hawa wanatokana na vumbi, chembechembe za vyakula zinazoangushwa, maji maji ya aina tofauti, wadudu wasioonekana, lakini pia inaelezwa kuwa mtu mmoja uangusha ngozi za miguu ziliyokufa Milioni 1.5.
2. Mkoba
Pia ni kitu kinachodaiwa kubeba bakteria wengi sana, haijalishi unatembea kwa miguu, au unatumia usafiri binafsi au wa umma ukiwa umetoka nao nyumbani.
Wanaotumia mikoba huiweka maeneo mbalimbali wakiwa kwenye matembezi yao ya kila siku, inaweza kuwa chini, kwenye meza ya mgahawa, sehemu ya kuwekea mikoba ukiingia chooni, kwenye kiti cha daladala na mengineyo.
Utafiti uliofanywa nchini Uingereza na kuchunguza mikoba 25, uligundua kuwa mikoba huwa ni michafu mara tatu zaidi ya kiti cha choo cha nyumbani.
3. Keyboard ya kompyuta
Kutokana na kukua na kusambaa kwa teknolojia duniani, kumekuwa na ongezeko la idadi kuwa ya watu kutumia kompyuta kwa namna moja au nyingine katika shughuli zao za kila siku na hii huweza kuwa nyumbani au ofisini na maeneo mengine.
Keyboard ya kompyuta yako inaweza kukupa ugonjwa kutokana na vimelea vinavyotokana na vumbi, chembechembe za mabaki ya chakula, mikono michafu ambayo ndiyo inatumia keyboard hiyo na vinginevyo.
Keyboard inatajwa kuwa na bakteria mara tano zaidi ya wanaopatikana kwenye kiti cha choo chako na hivyo inashauriwa kusafisha kompyuta na keyboard mara kwa mara, angalau mara 1 kila wiki.
4. Simu ya mkononi
Hiki pia ni kitu kinachotajwa kuwa na uchafu mwingi zaidi ya unaopatikana chooni. Kwanza kabisa hii ni kwasababu katika mazingira mbalimbali, unapeana na kushikana mikono na watu wengi na haujui usafi wa mikono yao.
Watu wengi hutumia simu zao karibu sehemu yotote, hata wakiwa chooni na hii huwaweka kwenye hatari ya kuambukizwa magonjwa.
Mwaka 2013 watafiti walifuta tablet 30, simu 30 na kiti cha choo cha ofisini ili kujua kila kimoja kinabeba uchafu kiasi gani.
Matokeo ya utafiti huo ni kwamba tablets zilikuwa na hadi bacteria 600 aina ya staphylococcus ambao husababisha magonjwa ya tumbo, simu zilikuwa na bakteria 140 na choo bakteria 20.
5. Sponji la jikoni
Utafiti uliofanywa na wanasayansi kwa sponji ya jikoni uligundua kuwa sponji hizo zinabeba bakteria aina 362 tofauti.
Utafiti mwingine uliofanywa na watafiti wa Arizona ambao ulikusanya madodoki na sponji 1,000 ya jikoni uligundua kuwa 10% ya yote ya bakteria aina ya salmonella.
Kutokana na hili inashauriwa kuwa, kila wiki loweka dodoki na sponji ya kusafishia jikoni kwenye maji ya moto angalau mara moja.
Maamuzi ameyachukua Naibu Waziri wa Elimu kwa Mwalimu Mkuu
Barua ya Hussein Bashe kwa Bunge “umoja, usalama wa Taifa”