Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo April 1, 2018 ameungana na Wakristo wote Tanzania katika maadhimisho ya Misa Takatifu ya sikukuu ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jimbo Kuu la DSM.
Misa hiyo imeongozwa na Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Joseph Padre Venance Tegete.
Akizungumza baada ya kukaribishwa na Padre Tegete kutoa salamu, Rais Magufuli amewatakia Watanzania wote heri ya Pasaka na ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuishi kwa amani na upendo huku wakishiriki ipasavyo katika ujenzi wa Taifa.
“Kifo na ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo ukafufue matendo yetu, tuendelee kuijenga amani yetu, upendo wetu na tujenge maendeleo ya Watanzania wote, kwani Kristo alifundisha upendo miongoni mwetu.” -Rais Magufuli
“Kwa hiyo Baba nakushukuru sana kwa kuongoza Misa hii, naomba ufikishe shukrani zangu kwa Kardinali Pengo, Maaskofu wote na Watanzania wote tuendelee kusimama pamoja ili kulijenga Taifa letu” –Rais Magufuli.
MAGAZETI LIVE: Nyundo za Maaskofu zaitesa Serikali, CHADEMA wahamia Gerezani