Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz, leo December 20, 2017 amezungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kinachoendelea kwenye upelelezi juu ya kupotea Ben Saanane na Mwandishi wa Mwananchi Azory Gwanda pamoja na waliomshambulia kwa risasi Tundu Lissu.
Kuhusu mwandishi aliyepotea ameeleza kuwa wamekwisha chukua hatua inayostahili kuchukuliwa pindi mtu anapopotea hivyo watu wawe na subira.
Suala la Ben Saanane amesema Jeshi la Polisi haliwezi kuweka wazi kila hatua wanayochukua kwenye upelelezi lakini tayari wameshachukua hatua zote za muhimu kumtafuta na kwamba kama kuna raia ana taarifa zozote za kusaidia upepelezi azitoe.
“Kwa taratibu zetu tunachukua kila hatua inayostahili kuchukuliwa wakati wa utafutaji wa mtu aliyepotea, zipo taratibu kwa hiyo tuwe na subira, swala la Ben Sanane sisi kama wapelelezi hatuwezi kusema kila hatua tunayochukua,” – Boaz
Alimalizia kwa suala la Lissu kwa kusema Jeshi la Polisi linalichukulia suala hilo kwa umakini na wanachukua hatua zote zitakazowezesha kupatikana kwa waliohusika na tukio hilo.
KWA WATAOSAFIRI KWENDA MIKOANI IWAFIKIE HII KUTOKA SUMATRA