Upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia hasara serikali ya Sh.bilioni 2.4 inayomkabili Mkurugenzi wa Tathmini ya Madini, Archard Kalugendo na mwenzake umekamilika.
Mbali ya Kalugendo, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo iliyopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ni Mthamini wa Madini ya Almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu.
Wakili wa serikali, Wankyo Simon alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa shauri limeitishwa kwa ajili kutajwa na upelelezi umekamilika.
Pia Wankyo alidai kuwa kuna baadhi ya vitu vinapaswa kukamilishwa katika kesi hiyo ikiwemo kusubiri uamuzi kama ikasikilizwe Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ‘Mafisadi’ ama lah.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi January 17, 2018.
MAHAKAMANI: Ilivyokuwa kesi ya madini ya almasi leo
KESI YA MADINI YA ALMASI: Mahakamani tena leo