Rais wa zamani wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud ameripotiwa kukataliwa kupewa visa ya kuingia nchini Marekani ambapo alitarajiwa kwenda kufundisha siku ya kesho March 27, 2018.
Mohamud alitakiwa kwenda kufundisha somo lililo na kichwa cha habari ‘Njiapanda Somalia: Fursa na Changamoto baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe’.
Mohamud ambaye alikuwa Rais wa Somalia tangu mwaka 2012 hadi 2017 amenyimwa visa hiyo kutokana na sheria mpya ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kuzuia baadhi ya mataifa duniani kutoingia Marekani.
Sheria hiyo ilianza kutumika mwaka jana na Somalia ni mojawapo ya nchi tatu za Kiafrika ambazo zimezuiliwa kuingia Marekani, nyingine ni Libya na Sudan.
BREAKING: Abdul Nondo aachiwa kwa dhamana Iringa